Duniani kuna mengi yanayo shangaza, Tumezoea kuangalia movie za "Vampire" na wakatimwingine kujiuliza ni za ukweli au nizauwongo. Leo naona nikuletee mwanamke ambaye ankunywa damu kama sisi wengine tunavyokunywa maji.Mwanamke mwenye umri wa miaka 29 ameasirika kwa kunywa damu "Fresh blood" ambapo hawezi kuacha kama ilivyo huwezi kuacha kunywa maji.
Michelle mwanamke ambaye ameanza kunywa damu ya Nguruwe iliyo fresh tangu akiwa mtoto na kwasasa hawezi kuacha kabisa kwani ndiyo inampa furaha maishani mwake. Mwanamke huyu anapatikana huko Lancaster, California.
"Damu ni muhimu kwangu kama ilivyo maji (Blood is as important as water to me)" Amesema mwanamke huyo. Pia amezidi kueleza kuwa kwake yeye anapokuwa ana soma vitabu, Anaangalia Television au kuchora/kupaka rangi ni mda hamana mda m'baya kwake kwenye kunywa damu.
Anazidi kufafanuwa maisha yake na unywaji wa Damu yakwamba hawezi kula chakula akakiona ni kizuri au kuamka asubuhi bila kunywa damu kwani ndiyo inampa nguvu. Wakati mwingine ili aone chakula nikizuri inamlazimu kupika chakula na kuichanganya ile damu kwenye hicho chakula ili kiwe na mvuto anao uhitaji.
Kama ilivyo watumiaji wa pombe, Sigara na vitu vingine vyinavyoweza kuwapa furaha na kuchaguwa baadhi ya sigara au pia ipi ina laza nzuri, Michelle naye anachaguwa damu na kusema ipi ni nzuri kwake na ipi anakuwa akiinywa inamburudisha. Anaeleza kuwa damu kama ya Nguruwe na Ng'ombe inakuwa na laza nzuri kuliko ile ya kondoo.
Michelle anaeleza kuwa inapofika asubuhi na hajapata damu anakuwa na asira na hata hawezi kwenda popote pasipo kupata kinywaji chake, Kwa mahesabu ya damu aliyokunywa miaka kumi iliyopita hadi leo ni takribani ya galono 1,000.
Source Daily Post.
© 24Hours Mix | Infotainment site




